MAANDALIZI YA SIKUKUU YA PASAKA YAANZA MAPEMA HUKO DODOMA, TAZAMA PICHA HIZI UONE


IMG-20140316-WA0001_2b472.jpg

Na Isabella Thomas - Dodoma
Katika hali ya kushangaza kwa kila kipindi tunachoelekea msimu wa sikukuu kumekuwa na uhaba mkubwa wa vitoweo hususani kuku katika maeneo mengi hasa ya mijini. 

Hali hii imejitokeza katika soko kuu la Majengo mjini Dodoma.

Kumekuwa na upungufu  wa kuku wanaouzwa kama kitoweo, hali hii imeonekena kwa kile kinachodaiwa kuwa wafugaji wanaouza kuku kwa jumla wamewahifadhi kuku hao huku wakilenga kuwauza katika sikukuu ya pasaka wiki tano zijazo kwa lengo la kupata faida zaidi. 

Hali hii pia imejitokeza ktk maeneo mengine ya masoko madogo mjini Dodoma.
IMG-20140316-WA0003_9cbaf.jpg
Kuku wakiwa wamehifadhiwa katika mabanda yao tayari  kwa mauzo ya msimu wa sikukuu ya Pasaka wiki tano zijazo
PICHA NA MJENGWA BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo