KUWASILI KWA MWILI WA MAREHEMU RC TUPA NYUMBANI KWAKE WILAYA YA KILOSA

Mzee Gabriel Tupa ( kulia) baba wa Marehermu John Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akitafakari jambo kabla ya mwili wa mwanae hakujawasili Machi 28, mwaka huu nyumbani kwake mjini kilosa  kwa ajili ya mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ( watatu   kushoto )  pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elisa Tarimo ( wapili kushoto )  wakisaidiana na  wananchi wa Kilosa kuweka kwenye meza jeneza lenye mwili wa marehemu John Tupa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara , nyumbani mwake Mjini Kilosa, baada ya kuwasili Machi 28, mwaka huu kutoka Mkoa wa Mara kwa ajili ya mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ( mwenye suti ) akisadiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elisa Tarimo ( mwenye shati la kitenge  ) na  wananchi wengine wa  Kilosa kuweka kwenye meza jeneza lenye mwili wa marehemu John Tupa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara , nyumbani mwake Mjini Kilosa, baada ya kuwasili Machi 28, mwaka huu kutoka Mkoa wa Mara kwa ajili ya mazishi
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, ( mwenye miwani) na ujumbe wake kutoka Mkoa wa Mara na Dodoma baada ya kuwasili na jeneza la mwili wa  Marehemu John Tupa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara , nyumbani kwake Mjini Kilosa, mkoani Morogoro , Machi 28, mwaka huu kwa ajili ya mazishi.
Picha zote na John Nditi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo