ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ILIVYOKUTANA NA CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU WAKATI AKIELEKEA KUKAGUA UPANUZI WA CHANZO CHA MAJI RUVU CHINI


Gari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Meck Sadicky likinasuliwa kwenye tope baada ya kukwama katika kijiji cha Mataya-Ruvu Chini,yote hiyo ikiwa ni sehemu ya changamoto ya Miundo mbinu hasa barabara,Wakati wakiongoza msafara wa Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa anakwenda kukagua chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea upanuzi wa chanzo hicho mapema jana jioni;wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.
Utaratibu wa kulinasua ukiendelea.
OOppss..haya twendeeeee....!
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh.Mecky Sadicky akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,mara baada ya kukumbana na changamoto ya miundombinu,wakati wakielekea  kukagua chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea hali halisi na kazi kubwa inayofanyika ya upanuzi wa chanzo hicho mapema jana jioni,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.
 Wakitafakari namna ya kupita mara baada ya kukutana na changamoto ya miundombinu,hasa barabara kama uonavyo pichani Lori likiwa limeziba njia kutokana na hali ya mvua kunyesha eneo hilo.  
 Gari ya Msafara ikinasuliwa kwenye tope . 
 Wadau kutoka Shirika la Utangazaji,TBC,Mtangazaji Elisha Elia  na Camera Man wake wakirekodi changamoto za miundombinu zilizoikubwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa anakwenda kukagua upanuzi wa chanzo cha maji Ruvu chini mapema jana jioni.

 Nyenzo ya kuongeza nguvu ikiwakwa sawa.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh.Idd Azan akizungumza jambo na mkulima wa Mpunga katika kijiji cha Mataya mapema jana jioni,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo