Msanii Jacqueline Wolper, amesema anaumizwa sana na tetesi
zinazozagaa kama moto wa kifuu kitaani kuwa anajihusisha na vitendo vya
usagaji.
Akizungumza nasi kuhusiana na skendo hiyo, mwanadada huyo
alisema, akiwa kama mwanamke anayejitambua na kumtukuza vyema Mungu
wake jambo hilo limekuwa likimuumiza.
“Roho inaniuma sana kuhusiana na hizo taarifa sijui niongee nini ili
jamii inielewe kile nitachokizungumza, ni ngumu sana kufanya hicho kitu
ambacho najua hakimpendezi Mungu kivyovyote vile,” alisema Wolper.