HALI YA MTANGAZAJI SALUM MKAMBALA WA CHANNEL 10 INAENDELEA VIZURI BAADA YA KUPATA AJALI YA GARI


HALI ya Mtangazaji wa Channel 10, Salumu Mkambala aliyepata ajali jana alfajiri kwa kugongana na lori akiwa safarini kuelekea Morogoro inaendelea vizuri katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza na mwandishi wetu hospitalini hapo, mdogo wa mtangazaji huyo, Ramadhani Mkambala alisema kaka yake alikuwa akielekea Morogoro na alipofika maeneo ya Vigwaza aligongana na lori alfajiri ya jana saa 10. 30 akiwa yeye na mtu mmoja aliyempa lifti.

Hata hivyo, chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na Ramadhani kuwa ni kutokana na barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo mengi hali iliyosababisha gari la kaka yake kuhama upande wake na kulivamia lori.

(PICHA, VIDEO NA HABARI: DEOGRATIUS MONGELA / GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo