BREAKING NEWS: WAWILI WAUAWA KWA RISASI WAKIWA WANASALI KANISANI NCHINI KENYA

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Joy Jesus wakiwa nje ya kanisa baada ya shambulio hilo.

WATU wawili wameuawa wakati wengine kumi wakijeruhiwa baada ya mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki kuwafyatulia risasi ndani ya kanisa la Joy Jesus huko Lokoni, karibu na Mombasa nchini Kenya.

Maafisa wa polisi katika wilaya ya Likoni iliyopo kusini mwa Mombasa wamesema kuwa jambazi huyo alilivamia kanisa hilo na kuanza kuwafyatulia risasi waumini hao kiholela.

Bado haijafahamika kama muuaji huyo ana uhusiano na vikundi vya kigaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo