AZAM YAITANDIKA SIMBA 2-1 HUKU YANGA NAYO IKIPEWA KIPIGO HICHO HICHO NA MGAMBO



Mgambo 2-1 Yanga
Azam 2-1 Simba
Mbeya City 1-0 Prisons

Michezo miwili iliyokuwa ikifuatiliwa na wapenzi wa mpira wa miguu nchini imemalizika kwa watani wa jadi kujikuta wakipoteza michezo yao. Katika mchezo uliofanyika uwanja wa Mkwakwani, mabingwa watetezi Young Africans Sports Club wamefungwa na maafande wa Mgambo kwa mabao ya Fully Maganga (dakika 1) na Malima Busungu (Dakika 69, penati) wakati bao la Yanga lilifungwa na nahodha Nadir Haroub katika dakika ya 50 kwa mkwaju wa penati. 
 
Katika mchezo huu Mchezaji wa Mgambo Mohammed Neto alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kukataa kukaguliwa baada ya wachezaji wa Yanga kulalamika kuwa amebeba kitu kilichohisiwa kuwa hirizi.

Uwanja wa Taifa vinara wa ligi Azam wameendelea kujichimbia kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wekundu wa Msimbazi Simba kupitia mabao ya Khamis Mcha (Dakika ya 16) wakati Simba wakisawazisha kabla ya mapumziko kupitia kwa Joseph Owino wakati John Bocco aliwahakikishia Simba ushindi kwa bao maridadi katika dakika ya 56.

Msimamo wa Ligi unafuatia hivi punde.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo