Na Pamela Mollel,Arusha.
Wahitimu
katika chuo cha Biashara na Teknohama Arusha(IBICTA)wametakiwa
kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutafuta masoko nje ya nchi kwaajili
ya kutangaza bidhaa za Tanzania hali itakayo saidia uchumi wa Taifa
kuwa juu
Wito
huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Sila( SILA VOCATION
TRUST ARUSHA) Bw. Adam Shayo juzi wakati alipokuwa mgeni rasmi katika
mahafali ya kwanza chuo cha Biashara na Teknohama Arusha
Alisema
kuwa changamoto kubwa iliyopo ni pamoja na bidhaa za Tanzania
kutotambulika katika soko la kimataifa huku akidai kuwa asilimia kubwa
ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zinaubora ukilinganisha na nchi
zingine
Aidha
aliwata wahitimu kutumia stashahada zao katika kuelimisha jamii kuhusu
umuhimu wa kutafuta masoko nje ya nchi kwaajili ya bidhaa zinazozalishwa
hapa Nchini
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Bw.Valentune Ndanu alisema kuwa
waliohitimu katika chuo hicho ni wanafunzi 10 huku akidai kuwa elimu
waliyoipata wahitimu hao itawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi wa hali
ya juu
Pia
alitaja faida nyingine watakayofaidika nayo ni pamoja na kutambua
fursa zilizopo sanjari na kujiingiza katika ujasiriamali hali
itakayowasaidia kuwa na ajira ya kudumu
Malengo ya chuo hicho ni kutoa digrii ya biashara na teknohama hali itakayosaidia vijana kujiingiza katika ujasiriamali,