Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya redio duniani, maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma ambapo redio zimeaswa kuacha tabia ya kupiga miziki isiyo na maadili kwa watanzania
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. rehema Nchimbi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo wakati akizungumza kwenye ukumbi wa Dodoma Hotel
Pia Dkt Nchimbi amekemea watangazaji kuacha matamshi yanayowafanya wanawake kuacha kusikiliza redio kwani nao wana haki ya kusikiliza redio
kauli mbiu ya mwaka huu ni "tusherehekee ushiriki wa wanawake katika redio na wote wanaowawezesha"
Na Veronica Mtauka, Dodoma.
