Video ya wimbo wa Shakira ‘Cant Remember to Forget You’ aliyompa
shavu mwimbaji mwenzake wa Caribbean, Rihanna imekosolewa vikali na
mwanasiasa mmoja nchini Colombia anayefahamika kwa jina la Marco Fidel
Ramirez, akidai kuwa kinyume cha maadili na hivyo kuwaharibu watoto
wadogo.
Marco Fidel, ameiomba serikali ya Colombia kuipiga marufuku video
hiyo ama vipande vya video hiyo ambavyo amedai kuwa vinasapoti usagaji,
uvutaji sigara na mauaji.
“Our Shakira with her erotic video is promoting tobacco usage and has
become the wost example for our youth.” Alitweet mwanasiasa huyo kutoka
Bogota, Colombia.
“Shakira’s new video is a shameless case for lesb**nism and
immorality. It is a danger to children. It sends a provocative message
to weak people who can be polluted and inducet to practice lesbian**m.”
Aliongeza katika tweet nyingine.
Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akijiita mlinzi wa kanuni na thamani,
aliwahi pia kuzikosoa baadhi ya video nchini humo kwa madai ya kutofuata
maadili.
