DK. JOSE CHAMELEONE AJICHORA TATOO YA JINA LA MKEWE SHINGONI



Wakati tunaelekea katika ile siku inayoaminika kuwa siku ya wapendanao ‘Valentine’s Day’, mkali wa Valuvalu Jose Mayanja Chameleone ameamua kumuonesha mkewe Daniella na dunia nzima jinsi anavyompenda, kwa kujichora tattoo yenye jina lake shingoni.
 
Chameleone ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa shughuli za kimuziki, alipost picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, picha zinazoonesha tattoo hiyo hata mtu akimuona kwa mbali kidogo.
 
Mwimbaji huyo wa Valuvalu ambaye ana watoto watano aliozaa na mkewe Daniella hakuwasahau wanae pia, alijichora katika mkono wa kushoto tattoo yenye majina manne ya wanae wanne na anatarajia kuongeza moja yenye jina la mwanae wa kwanza, Ayla.
 
“2014 we stand tall for the ones we care for and those that love us back with their whole. For me, this is my expression..” Amesema Chameleone.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo