TOGOLANI MAVURA ATEULIWA KUWA MSAIDIZI WA RAIS KITENGO CHA HOTUBA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Togolani I. Mavura (pichani) kuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba) kuanzia Februari 8, mwaka huu, 2014.

Taarifa iliyotolewa Jumanne, Februari 25, 2014, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Bwana Mavura anachukua nafasi ya Bwana Msafiri Marwa ambaye amehamishimiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kupangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mavura ambaye ni Ofisa wa Mambo ya Nje alikuwa Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo