JESHI la Polisi Zanzibar, jana limetoa ufafanuzi wa matukio ya milipuko iliyotokea katika maeneo manne tofauti.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Hamdani Omari Makame,
alisema tukio la kwanza lilitokea Februari 23 mwaka huu, saa saba mchana
eneo la Pangawe.
Alisema mlipuko huo ulitokea baada ya waumini wa dhehebu la Evengilistic kumaliza ibada na haukuleta madhara yoyote.
Aliongeza kuwa, wakati polisi wakishughulikia tukio hilo, saa 6:36 mchana ikatokea milipuko mingine mitatu katika maeneo mawili tofauti.
Aliongeza kuwa, wakati polisi wakishughulikia tukio hilo, saa 6:36 mchana ikatokea milipuko mingine mitatu katika maeneo mawili tofauti.
"Mlipuko
wa kwanza ulitokea eneo la Malindi mjini Zanzibar kwenye Mkahawa wa
Mercury unaomilikiwa na Bw. Simai Mohammed Saidi (45) lakini haukuwa na
madhara.
"Ilipofika
saa 8:35 na 8:40 kwenye mtaro mmoja uliopo karibu na Mkunazini, eneo la
Mji Mkongwe, Mjini Zanzibar ilitokea milipuko miwili iliyopishana kwa
muda wa dakika chache," alisema.
Alisema
milipuko hiyo pia haikuleta madhara kwa binadamu isipokuwa gari moja
lenye namba Z.355 ET Harrier mali ya Bw. Mohammed Ibrahim Ali,
lililoegeshwa karibu ya mtaro lilipata madhara kidogo kwa kutoboka bati
upande wa nyuma kulia.
Kamishna
Makame alisema milipuko yote ilitengenezwa kienyeji na Polisi kwa
kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
wamechukua mabaki ya milipuko hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa
kitaalamu.
Aliongeza
kuwa, polisi wameimarisha doria katika maeneo mbalimbali ndani na nje
ya Zanzibar ili kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena na kuweza
kuwakamata wahalifu hao.
"Tayari
timu ya Makachero wakiwemo Wataalamu wa Uchunguzi wa Kisayansi kutoka
Makao Makuu ya Upelelezi, Dar es Salaam, wamewasili mjini Zanzibar
kuungana na Makachero wenzao wa Zanzibar kuendelea na uchunguzi huu,"
alisema.
Alisema
katika hali isiyo ya kawaida, Mkoa wa Kusini Unguja, juzi saa nane
mchana katika Kijiji cha Unguja Ukuu, eneo la Kae Pwani, kulikuwa na
wavuvi wakivua vyuma ili kwenda kutengeneza nanga ya boti lao, lakini
wakati wakiendelea na kazi hiyo chuma walichokuwa wakikitengeneza
kililipuka na kujeruhi watu wanne.
Waliojeruhiwa
na kukimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ni Juma Abdallah Juma (32),
Shabani Khamisi Ibarahim (32) Haji Khamisi(35) na Sumai Hussein Hassan
(38).
Wakati
majeruhi hao wakiendelea na matibabu, majeruhi mmoja Juma Abdallah Juma
(32) alifariki dunia saa 11 jioni na mmoja kati yao Sumai Hussein
Hassani (38) alitibiwa na kuruhusiwa ambapo wengine wawili wanaendelea
na matibabu.
