Wanafunzi
wa chuo cha taaluma ya polisi Moshi wakijaribu kuzima moto na kuokoa
mali zilizokuwa zikiungua katika moja ya stoo ya kuhifadhia vitu
mbalimbali zikiwemo nguo baada ya kuzuka kwa moto katika jengo hilo.
Hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika na Mkuu wa Chuo hicho Kamishana Msaidizi wa Polisi Matanga Mbushi ameahidi kutoa taarifa kamili baadaye.

Askari wanafunzi wakipambana na moto kwa kila jinsi

Mapambano na moto yanaendelea

Baadhi ya vitu vikiokolewa kutoka katika jengo lililowaka moto.

Juhudi za kuondoa vifaa vilivyookolewa kabla ya kuteketea kwa moto

Wanafunzi wakipambana na moto






Sare za askari zikiwa zimeokolewa toka katika jengo hilo.

Moja
ya kifaa kilichopo chuoni hapo ambacho pia kilikuwa kikitumika kwa
shughuli za kuzima moto katika jengo hilo


Kamanda
wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akiwa na mkuu wa Chuo cha
taaluma ya Polisi kamishana msaidizi wa polisi Matanga Mbushi
wakishuhudia zoezi la uzimaji moto katika jengo hilo.




