Mganga
mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dk.Kitundu Jackson ,akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari juu ya mapokezi ya majeruhi wa basi la
bunda lililogonga kichwa cha Treni leo.Picha zote na Nathaniel Limu.
Bbasi
la Bunda lililokuwa likitokea mjini Dodoma linakwenda jijini Mwanza na
kugonga kichwa cha Treni maeneo ya mjini Mnayoni,linavyoonekana katika
picha baada ya kugonga.
Baadhi
ya majeruhi wa basi la Bunda lililogonga kichwa cha Treni mjini
Manyoni,wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya
Manyoni.
Na Nathaniel Limu, Manyoni.
AFISA
Mstaafu wa NMB benki tawi la Manyoni mkoani Singida ambaye kwa sasa
alikuwa Mhasibu wa SACCOS ya chama cha walimu Tanzania Manyoni,Belida
Kombo amefariki dunia baada ya basi la kampuni ya Bunda alilokuwa
akisafiria kugonga kichwa cha treni na kujeruhi abiria wengine 39.
Basi
hilo T.782 BKZ aina ya scania lililokuwa Farak Adamu lilikluwa
likitokea Dodoma mjini kuelekea jijini Mwanza,liligonga kichwa cha treni
eneo la makutano ya barabara kuu ya Dodoma – Singida na reli eno la
round about ya Manyoni mjini leo saa moja na nusu asubuhi.
Bi
Kombo ambaye alipandia basi hilo katika kituo cha mabasi cha Manyoni
mjini na alifariki dunia dakika chake wakati akihangaika kutafuta
kiti.Pia ndugu zake waliomsindikiza wakiwa bado hawajaondoka eneo lam
kituo cha mabasi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya
Manyoni,Dk.Kitundu Jackson amekiri kwamba amepokea majeruhi 39 wa ajali
ya treni na basi na kati yao sita wana hali mbaya. Amesema
majeruhi walio na hali mbaya ni pamoja na kondakta wa basi Masage
Bunyema na kwamba baadhi watapewa rufaa ya kupelekwa hospitali ya mkoa
wa Dodoma na wengine katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi.
“Tayari majeruhi wawili tumeisha wapa rufaa kwenda kupata matibabu
katika hospitali ya mkoa ya Dodoma mjini na sista mmoja tumempeleka
katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi”,alifafanua zaidi
Dk.Kitundu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatma Toufiq ameiangiza
mamlaka ya TRL na TANROADS kujenga haraka kuweka mtumishi wa kutoa
angalizo kwa vitambaa juu ya gari la moshi linapopita katika eneo hilo
ambali kumetokea ajali tatu katika kipindi kifupi kilichopita.
Aidha,mashuhuda
wa ajali hilo,wamedai kuwa hicho kichwa cha treni kilichokuwa kikitokea
katika kijiji cha Aghondi,dereva wake alijitahidi kupiga honi kali ili
kumwonya dereva wa bunda basi lakini dereva huyo hakujali.Kama
haitoshi,dereva wa hiece aliyekuwa apishane na basi hilo,alimumulika kwa
taa akimwonya asimame ili kipisha kichwa hicho,lakini hakujali pia.
Watu
hao wamedai kuwa dereva wa basi hilo alikuwa kwenye mwendo kasi wakati
akipewa onyo hilo la kupisha kichwa cha treni lipite.