IGP Sirro amesema hayo leo alipokuwa mkoani Mtwara na kuwataka wahalifu hao waliokimbilia mkoani Mtwara kuacha mara moja vitendo vya uhalifu walivyokuwa wakifanya Kibiti kabla ya jeshi la polisi kuwatia nguvuni.
Mkoani Pwani zaidi ya watu 30 walifariki dunia wakiwepo viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, askari polisi na raia wengine kwa kuuwawa na watu wasiojulikana ambao walikuwa wakifanya uhalifu huo na baadaye kuzibitiwa na jeshi la polisi huku wahalifu wengine wakisemekana kukimbia katika maeneo hayo na kukimbilia mkoani Mtwara
