skip to main |
skip to sidebar
MWIGIZAJI SHAMSA FORD AUGUA KICHAA
Stori:SHANI RAMADHAN MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa aliwahi kuugua ukichaa.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na mtoto wake wakiburudika.
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Shamsa alisema
ukichaa huo aliupata alipokuwa akisoma kidato cha pili katika Shule ya
Sekondari Kunduchi-Beach, jijini Dar ambapo alilazimika kukaa nyumbani
kwa takriban mwaka mzima kupatiwa matibabu.
Akifafanua
zaidi kuhusiana na ugonjwa huo, mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto
mmoja, alisema ulimtokea ghafla, alijikuta ameanza kushikashika vitu
hovyo, kuzungumza maneno yasiyoeleweka ndipo wazazi wake walipoamini
amepatwa na tatizo la akili.
Alipelekwa hospitali na kupewa dawa za kutumia na zaidi anamshukuru
Mungu, mama yake ni mshikadini, kwani alimuuombea hadi akapona na
kuendelea na masomo kwa kurudia kidato cha pili.
“Nilikuwa ni mtu wa kuhangaika mara huku mara kule, yani naongea vitu
ambavyo havipo, lakini namshukuru sana Mungu alinisaidia baada ya
kuzunguka sana na mama pamoja na ndugu zangu waliokuwa wakiniombea dua,
nilipona kabisa,” alisema Shamsa.
Kuna wakati akiwa katika hali hiyo, Shamsa alifikia hatua ya kujisaidia haja zote bila kuvua nguo.
“Akili haikuwa yangu, niliweza kufanya kitu ambacho nilikatazwa,
nilikuwa nikirudia mpaka nikawa nalindwa, sikuachwa peke yangu hata
dakika moja” alisema staa huyo ambaye yuko katika mchakato wa kufunga
pingu za maisha na mzazi mwenzake, Dick.
SOURCE: GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi