MWANAMKE ANASWA NA MAFURUSHI YA BANGI ZANZIBAR


 picha na maktaba
 
Na Masanja Mabula, PEMBA — 
 
JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, linamshikilia mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mwanaisha Kiyaka Ayoub (30) mkaazi wa Pande Tanga na Chake Chake kwa tuhuma za kupatikana na mafurushi ya bangi.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Mlenge Mohammed Mlenge, alisema mtuhumiwa alikamatwa jana majira ya saa 11:50 alfajiri baada ya kushuka kwenye mashua katika bandari ya Wete akitokea Tanga.


Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi la polisi.
 
Taarifa za kwamba kuna mtu anakuja na bangi tulizipokea mapema na kuweka mtego hapa bandarini Wete, kwa kweli haikuwa shida kumkata alisema.

Aidha alisema baada ya kufanya upekuzi kwenye begi lake walimkutana mafurushi 22 ya bangi.
 Aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono falsafa ya polisi jamii ambayo imekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na matendo ya uhalifu. Alisema polisi wanaendelea kukamilisha uchunguzi kabla ya kumfikisha mahakamani. --- via ZanziNews
>>..wavuti


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo