MVUA kubwa ilionyesha usiku wa kuamkia leo zilifunga baadhi ya mitaa
kwa kujaa maji jambo ambalo lilileta hofu kwa wananchi na baadhi kuamka
na kuangalia usalama wao endapo mvua hizo zitaleta maafa. Mvua hizo
zilifunga baadhi ya mitaa eneo la Tabata Bima na kuleta maafa kwa maji
kuingia baadhi ya nyumba eneo la Bonde la Mto Msimbazi. Mwandishi wa
Thehabari.com alishuhudia baadhi ya mitaa ikiwa umejaa maji na njia
kufunikwa kabisa na maji huku baadhi ya wananchi wakiamka usingizini
kuangalia usalama wao.
Maji yaliingia kwenye baadhi ya nyumba za watu wa bonde la Msimbazi
jambo ambalo liliwalazimu wakazi hao kuanza kutoa baadhi ya vyombo nje
ili visisombwe na maji ya mvua yaliyokuwa yakivamia kwenye nyumba zao. Chini ni picha mbalimbali zikionesha namna baadhi ya mitaa ilivyo jaa maji na njia za mitaa kufunikwa kabisa.
Picha
mbalimbali zikionesha namna baadhi ya mitaa ilivyo jaa maji na njia za
mitaa kufunikwa kabisa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha usiku wa
kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa
Thehabari.com