MVUA YAUA WANAFAMILIA TUNDUMA MBEYA

MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani hapa zimesababisha vifo vya watu watatu wa familia moja baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba walipokuwa wamelala.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Sogea, mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni baba wa familia hiyo, Steven Mwaijombe (35), mkewe Ester Kibona (25) pamoja na mtoto wao Edga Mwaijombe (2), wakazi wa Sogea.

Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha afya Tunduma kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Wakati huohuo, watu saba wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa kukutwa na pombe haramu aina ya gongo yenye ujazo wa lita 1.5.

Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wanakunywa pombe hiyo kutokana na msako wa kukamata watu wanaofanya biashara hiyo mkoani hapa.

Kamanda Msangi alisema taratibu za kuwafikisha mahakamani zinafanyika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo