OFM yamuokoa mtoto wa huyu.
Awali, OFM ilifika nyumbani kwa mama huyo maeneo hayo ya Tandika ili kujiridhisha na tuhuma hizo ambapo ilijionea jinsi mama huyo anavyomtumikisha na kumnyanyasa mtoto huyo.
Kwa mujibu wa majirani, mtoto huyo ambaye yupo chini ya umri wa miaka 18, huamshwa saa 11:00 alfajiri na kutakiwa kufanya kazi zote za ndani (isipokuwa kupika) na kwenda kuchota maji kwa mkokoteni kila siku, tena umbali mrefu huku ikidaiwa kuwa hufanya hivyo mara tatu au nne kwa siku bila kula.
Mtoto huyo akichoteshwa maji.
Ilidaiwa kwamba siku moja kabla ya kukamatwa kwa mwalimu huyo, mtoto huyo alipokea vipigo mfululizo kisa alimsindikiza jirani yake aliyeomba aende naye mahali.
Siku ya tukio OFM ilimtafuta mtoto huyo ambapo ilimkuta akijiandaa kwenda shule na kujionea jinsi alivyodhoofu na kujaa makovu mwilini.
Majira ya saa 11:00 jioni, OFM, ikiwa na polisi wa dawati la jinsia kutoka Mbagala-Kizuiani ‘iliseti’ mitego yake kila kona na kupata taarifa kuwa shangazi wa mtoto huyo ambaye ndiye anayedaiwa kuhusika na unyanyasaji huo, alikuwa tayari amerejea kutoka kazini hivyo kwa muda huo mtoto huyo angeanza kufanyishwa kazi ikiwemo kuchota maji jambo ambalo lilikuwa kweli.
Haraka, OFM ilimfuatilia mtoto huyo akiwa na tolori la maji lenye madumu manne hadi bombani ambapo mwenyewe alisema aliambiwa na shangazi yake, arudie kuchota maji mara nne, jambo ambalo lilikuwa kweli.
OFM ilimshuhudia mtoto huyo akijaza madumu ya maji na kulisukuma tolori hilo kwa tabu huku kila aliyemuona akiishia kumsikitikia jambo lililowalazimu OFM wamsaidie huku wakiongozana na polisi hao hadi nyumbani kwao na kumkamata mama huyo.
Akionesha ubabe wake, mwanamama huyo awatolea maneno machafu OFM na polisi waliokuwa eneo hilo na kudai kuwa yeye anafahamiana na watu wakubwa na kamwe hawezi kwenda rumande.
Hata hivyo, baada ya kuona mambo yanakuwa magumu, mama huyo alikubali kuelekea kituoni ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba MBL/RB/1827/2014- UNYANYASAJI huku mtoto huyo akiwekwa chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii.
CHANZO:GPL