MSAKO WA STIKA ZA MAGARI NA PIKIPIKI KUANZA BAADA YA FEBRUARI 25 MWAKA HUU NJOMBE MJI

Na Gabriel  Kilamlya Njombe
Halmashauri ya Mji wa Njombe Kwa Kushirikiana na Wakala wa Ukusanyaji Mapato na Stika za Vyombo VyaMoto Imesema Itawachukulia Hatua za Kisheria Wamiliki Wote wa Vyombo Vya Moto Ambao Hawajalipia Stika za Mapato  ya Vyombo Vyao.
Aidha Halmashauri Hiyo Imesema Inatarajia Kuendesha Oparesheni ya Kuwakamata Wamiliki  wa Vyombo Hivyo Ambao Walioshindwa Kulipia Stika Hizo Kwa Hiyari Hadi Kufikia Februari 25 Mwaka Huu .
Akizungumza na gabriel kilamlya blog Wakala wa Ukusanyaji Mapato na Stika Halmashauri ya Mji wa Njombe Zabron  Mgeni Amesema Hatua Hiyo Inakuja Kufuatia Idadi Kubwa ya Wamiliki wa Vyombo Vya  Moto Kukwepa Kulipia Vyombo Vyao Yakiwemo Magari na Pikipiki.
Bwana Mgeni Amesema Licha ya Baadhi ya Wamiliki wa Vyombo Hivyo Kulipia Mapato na Stika Lakini Baadhi Yao Wanaonekana Kukaidi Kulipia Ushuru Vyombo Wanavyo Vimiliki Yakiwemo Magari na Pikipiki , Ambapo Ameongeza Kuwa Kwa Wale Wote Walioshindwa Kulipia Stika Hadi Siku ya Februari 25 Mwaka Huu Watachukuliwa Hatua za Kisheria Ikiwemo Kulipa Faini ya Shilingi Elfu 50.
Hata Hivyo Bwana Mgeni Ametoa Wito Kwa Wamiliki wa Vyombo Vya Moto Kulipa Stika Kabla ya Tarehe Hiyo Ili Kuepuka Usumbufu Unaoweza Kujitokeza Pamoja na Faini.
  Suala la Ulipaji wa Stika za Magari na Pikipiki Linapaswa Kuwekwa Kipaumbele Katika Masuala Ya Kibiashara Hususani Katika Mitaa na Vijiji Vilivyopo Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo