skip to main |
skip to sidebar
LULU AYAKUMBUKA MAPENZI YA KANUMBA, SOMA ALICHOKISEMA
Stori: Mayasa Mariwata
WAKATI kesi yake juu ya
kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba ikianza
kurindima leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mwigizaji
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa la moyoni akikumbuka mapenzi ya jamaa
huyo aliyetangulia mbele za haki.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Siku ya Wapendanao
(Valentine’s Day) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa iliyopita.
Marehemu Steven Kanumba.
“Kuna mtu natamani kumtakia Happy Valentine’s Day kwa kuwa nakumbuka
mapenzi yake kwangu lakini kwa bahati mbaya siwezi kwa sababu hayupo na
haiwezekani tena,” alisema Lulu.
Hata
hivyo, alipobanwa amtaje, staa huyo ambaye ni sura ya mauzo ya filamu
za Kibongo alikiri kuwa ni Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012,
siku ambayo kamwe hawezi kuisahau maishani mwake.
CHANZO:GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi