*Barua ya kuomba kazi inaongelea kwa kifupi kuhusu wasifu wako na
kukujumuisha kama mtu anayehitajika kwenye kazi furani.*
Ni sehemu pekee ya kuonyesha unahitaji hiyo nafasi ya kazi na
kutengeneza uhusiano wako na mwajiri mtarajiwa. kuonyesha kwamba
unahitaji kazi hiyo kwenye barua ni muhimu sana, na kuna jambo moja
linalokuhakikishia utaitwa kwenye usaili.
Omba kukutana na Mwajiri au Mtu anayefanya Usaili.
Je waujua usemi unaosema, "Ombeni nanyi mtapewa"? Ni kweli. Linaweza
kuwa jambo la kawaida na ushauri wa kawaida bali ni mara ngapi umeandika
barua ya kuomba kazi bila kuomba kufanyiwa usaili? wakati ni rahisi kufanya!
Wakati unamalizia kuandika barua yako, kitu unachotakiwa kukifanya ni
kumuuliza mwajiri kuhusu kukwita kwenye usaili. Utafiti unaonyesha watu
wanaoandika kwenye barua na kuomba kufanyiwa usaili wana nafasi zaidi ya
kuitwa kuliko ukinyamaza kimya.
Unapomalizia barua yako kama ni Kiswahili sema,
"Nimevutiwa na nafasi ya kuwa Meneja Mauzo wa kampuni yenu na
ningependa kupata nafasi ya kukutana nawe ana kwa ana ili niweze
kuongelea uzoefu wangu na mchango wangu ninaoweza kuutoa kwa ajili
ya nafasi hiyo.
Tafadhali unaweza kunipigia kwenye simu namba
+255xxxxxxx na kunipangia lini unaweza nifanyia usaili kulingana na
wakati na nafasi uliyonayo kukutana nami."
Kuna namna nyingi unazoweza kuomba kuitwa kwenye usaili wakati
ukiandika barua ya kuomba kazi, hivyo jifunze zaidi na uongeze
nafasi yako ya kuitwa kwenye usaili