skip to main |
skip to sidebar
WAZIRI WA UHAMIAJI WA UINGEREZA AJIUZULU BAADA YA KUPONZWA NA MWANAMKE
Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper.
WAZIRI wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya
kugundulika kuwa amemuajiri mfanyakazi asiyekuwa na kibali cha kufanya
kazi Uingereza.
Harper ameeleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha
nyaraka za bandia, alipomuajiri mwaka 2007 kusafisha nyumba yake.
Bwana Harper ambaye amekuwa Waziri wa Uhamiaji tangu mwaka 2012,
alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu
uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine na
amemuomba radhi Waziri Mkuu, David Cameron kwa tukio hilo.
Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi