Mwanamuziki na muigizaji baby Joseph madaha amefunguka na kusema
kuwa kweli ameamini uchawi na kupigana juju vipo kwenye gemu kwani
mambo yaliyomtokea hivi karibuni haelewi hata imekauje.
Chanzo nini?
Hapo siku za nyuma baby Madaha alipatikana na dhahama ya
kukumbwa na kashfa nzito sana ya kujiuza kwa dau la milioni kumi kwa
jamaa mmoja hivi mitaa ya Dar es Salaam Jambo lilolopelekea yeye kupigwa
chini na Record label yake ya Candy and Candy ya huko Kenya na
kupokonywa gari aina ya AUDI TT aliyokuwa akitembelea huku akiharibu pia
uhusiano wake na bosi wa record label hiyo - Joe kairuki ambaye pia
anadaiwa kuwa mpenzi wake.
Je ni Kweli alijiuza?
Baby Madaha ambaye amerudi nchini hivi karibuni tokea Nairobi
alipoenda “ku-solve” ishu yake hiyo na label hiyo anasema yani hata
haelewi kitu gani kilitokea siku hiyo ingawa mpaka akaandikwa kama
alienda kujiuza, anachokumbuka ni kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu an
kumwambia anataka wafanye naye kazi ya kusambaza filamu yake mpya ya Gal
Bladder ambaye inatikisa soko kwa sasa.
Baada ya kufika hapo waliongea vizuri na kuondoka ghafla kabla
ya kuja kusoma kesho yake kuwa alikuwa anajiuza kitu ambacho ansema
hajui kimetoka wapi.
“Yani hata sielewi ilikuaje nikaenda kukutana na yule jamaa,
ilikuwa ni kama muujiza hivi, mwanzo nilisita sana ila nikashangaa
nimefika tu pale bila kujielewa, ni vitu vya ajabu sana” alieleza baby
Madaha.
Uhusiano wake na Label hiyo ukoje sasa?
Akizungumza na bongomovies, baby amesema kwa sasa kila kitu kipo
sawa kwani alipoenda Kenya waliongea vizuri na bosi wake huyo na
kumaliza tofauti zao na sasa amerudi nchini kusambaza filamu yake hiyo
mpya ya Gal bladder huku akijiindaa kupiga show kwenye tour yake
aliyoiandaa jina la Top Up and Refill itakayofanyika mwezi ujao wa
tatu.
Mwenyewe anasemaje zaidi?
Hata wafanyaje, waniroge, wanichafue, i'm a bad gal, na
sibabaishi na vijimaneno vya watu hata kidogo, sitoki candy and Candy
hata waloge kwa waganga wote duniani. Kama walifikiri nimeumbuka, wajue
watasubiri sana. Nikitoka kenya naenda Holywood tu!