AZAM FC YAIBAMIZA FERROVIARIO DE BEIRA YA MSUMBIJI BAO 1-0

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwAIJcZXitkWGIjTFLcUgvgKJZEk_yVS4C5HPtHMFSVXgPfCqGJGoRrNevX7IrG-cnwqUVhHbXjG1DYt3QdMumVXOipO9BUaM3A-U4K11KqQIONfz0VvwPbOIZAEcuazpC76-W4Lf0K4sp/s1600/kipre1.jpgHabari na picha na Mahmoud Zubeiry

AZAM FC imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.

Shukrani kwake mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche (pichani juu) aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 41 baada ya kutengewa pasi nzuri ya kichwa na Mganda Brian Umony na kufumua shuti kali.

Mchezo ulikuwa mkali dakika zote 90 na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgc_HV0oJd6K08v-l0g0839tcO73qgmQ9RLPQOEeWIJDosauCVveHMczKQo-V55vyLq2LTDIM9OaLbJLP3Z-sGtNlWtRapSb3ruO5ngSLj3vSH3Q9_OuzlQ4EIDcPIJQMJs-BZqh_YMucKm/s1600/kipre2.jpgKiungo mkabaji wa Ferroviario, de Beira akipiga tik tak dhidi ya mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umony leo Chamazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo