SIMBA YACHEZEWA SHARUBU NA MGAMBO JKT, YAPIGWA 1-0

Mgambo JKT

BAO pekee la dakika ya 28 lililofungwa na Full Maganga limetosha kuiua 'Mnyama' Simba inayonolewa na kocha mwenye mbwembwe, Zdravko Logarusic mbele ya Mgambo JKT katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara lililochezwa Mkwakwani Tanga.

Simba ambayo iliitafuna Mgambo iliyokuwa ikifundishwa na King Abdallah Kibadeni kwa mabao 6-0 licha ya juhudi za kutaka kurejesha bao hilo ilishindwa kabisa kuwapa raha mashabiki wake kwa kukubali kipigo cha pili kwa msimu huu na cha kwanza chini ya Logarusic tena kwa timu kibonde ya Mgambo.

Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Mgambo JKT ambayo ilikuwa ikiburuza mkia kwa kipindi kirefu baada ya wiki iliyopita kuicharaza Ashanti United uwanja wa cha Chamazi.

Ushindi huo umeifanya timu hiyo inayonolewa na kocha mpya Bakar Shime imefikisha pointi 12 huku Simba ikisaliwa na 31 na kushuka nafasi ya nne iliyokuwa awali baada ya Mbeya City kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Mbeya


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo