Silinde ambaye ni Waziri Kivuli, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Katika Taarifa yake kwa Vyombo vya Habari kuhusuMgogoro wa Ardhi Kiteto; amemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amshauri Rais awafukuze kazi Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wake.
WANANCHI wa Mvomero waliohojiwa kwa nyakati tofauti, wamempongeza Silinde kutumia nafasi
ya Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), wakiunga
Mkono watendaji hao watimuliwe baada ya kupata taarifa za kina , na
ikibidi aitaarifu na kuishauri Kambi ya Upinzani bungeni inayoongozwa na
CHADEMA, ichukue hatua za kibunge nje na ndani.
Walishauri, ni kweli lipo tatizo la
migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengi nchini, hivyo
Mbunge huyo na kambi yake ifike katika maeneo yaliyoathirika ili iongee
na waathika hao na kupata picha halisi ilyojiri kwa wananchi hao kwa
nchi nzima ili izitendee kazi kero hizo.
Katika Taarifa yake ya Januari
16, 2014 katika Mitandao ya Kijamii, Silinde alimtaka Waziri Mkuu,
Pinda, amshauri Rais Jakaya Kikwete awafukuze kazi Mkuu wa Wilaya,
Martha Umbulla, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Jane Mutagurwa
.
“Kutokana na mgogoro mkubwa wa ardhi kati
ya wakulima na wafugaji unaoendelea wilayani Kiteto ambao umefikia
hatua ya kusababisha maafa makubwa ya umwagikaji damu, mauaji ya watu na
uharibifu wa mali, Wizara Kivuli, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),
inatoa taarifa ifuatayo kwa umma;
“Tunamtaka Pinda atakapojionea kwa macho
athari za mgogoro huo umedumu kabla na baada ya mwaka 2006, achukue
hatua za kinidhamu kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Umbulla na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya, Mutagurwa, amshauri Rais Kikwete awafute kazi
wote wawili mara moja”.ilisema sehemu ya taaraifa hiyo.