skip to main |
skip to sidebar
TAZAMA VIDEO YA TAARIFA ILIYOSABABISHA MEYA WA BUKOBA KUJIUZULU
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa Maelezo ya
Serikali. Kuhusu Suruhisho hilo ambapo yamebainika Makosa ya Meya
Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya Madiwani na Taratibu za
serikali, Basi ajipime Mwenyewe na Kujiuzulu mara moja kwa Maslahi ya
Manispaa ya Bukoba.
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk Anatory Amani amejiuzulu wadhifa wake leo baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, (CAG) iliyosomwa kwenye Ukumbi wa Bukoba Town Council kuelekeza tuhuma zote za matumizi mabaya ya madaraka zinazoelekea kwenye ubadhirifu kuthibitika.
Vile vile, pamoja na viongozi wengine kuvuliwa nyadhifa zao kwa mujibu wa agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kama lilivyosomwa na Naibu Waziri, TAMISEMI, Aggrey Mwanri, dola imeagizwa ichukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika waliopoteza nyadhifa zao leo kwa makosa na hasara waliyosababisha.
Shukurani ya video kwa blogu ya BukobaWadau.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi