skip to main |
skip to sidebar
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM WAFANYA OPERESHENI YA KUSAKA WAFANYABIASHARA WA NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA
Januari
15 wafanyabiashara wa nguo za ndani wa soko la Karume hawakuimaliza
vizuri siku hii baada ya Shirikia la Viwango Tanzania[Tbs]kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini kuendesha operesheni ya Kataza
kuuza nguo za ndani ambazo zishatumika(mitumba).
Afisa
Habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi Roida ameongea na
waandishi wa habari mara baada ya kukamata kwa marobota hayo ya nguo za
ndani ambapo amesema wamekamata nguo hizo za ndani kwa sababu
walishazipiga marufuku kuuzwa hapa nchini kwa kukosekana kwa viwango
vinavyotakiwa lakini wafanyabiashara hao wamekua wakikaidi agizo hilo na
kuendelea kuuza.
Wafanyabiashara wa Karume wakiishuhudia hali hiyo.
Marobota ya nguo za ndani jana yalipakizwa kwenyemagari ya polisi na
yalielekea kituo cha polisi cha msimbazi kwa ajili ya kuteketezwa kwa
moto.

Baadhi ya nguo za ndani zilizokamatwa.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi