Mkurugenzi
huyo amesema Shirika la nyumba badala ya kwenda kutoa msaada wa sabuni
na vyakula katika vituo vya watoto yatima au kusaidia biskuti limeamua
kubadilisha maisha ya vijana wa Tanzania kwa kuwapa mafunzo na
kuwapatia mashine za kutengeneza matofali ya udongo ambayo wao NHC
watakuwa ndiyo wateja wakuu wa kununa matofali hayo, lakini pia shirika
hilo linatoa mashine za kufyatulia matofali zipatazo 640 katika wilaya
160 mikoa yote ya Tanzania bara na kiasi cha shilingi 500,000 kila mkoa
kama mtaji wa kununulia saruji kwa vikundi hivyo, Katikati ni Injinia
Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation
Housing&Building Research Agency
(NHBRA) na kushoto ni Bw.Julius Njelwa kutoka VETA, mafunzo hayo
yameratibiwa kwa pamoja na (NHC), (VETA) na (NHBRA) kwa pamoja.(PICHA NA
KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) akifafanua masuala ya kitaalamu kuhusu teknolojia hiyo ya matofali kwa waandishi wa habari. 
Baadhi
ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwa katika maadalizi hayo
kushoto ni Suzan Omary Meneja Mawasiliano NHC, Muungano Saguya Meneja
huduma kwa jamii NHC na Ephraim Kibonde mtangazaji wa Clouds Radio.