POLISI mkoani Mbeya, inawashikilia watu watano wakiwemo askari polisi na
magereza wawili kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ujambazi wa kutumia
silaha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, aliwataja askari
hao ambao wamejihusisha na tukio hilo kuwa ni askari namba B. 500 SGT,
Juma Musa wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Ruanda Mbeya na F.8302 PC
James wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbeya.
Alisema, tukio h ilo lilitokea juzi saa 11:35 jioni katika eneo la Mlima Kawetele barabara ya Mbeya-Chunya, ambapo askari hao walikuwa na wenzao watatu ambao ni raia, Mbaruku Hamisi, Amri Kihenya na Elinanzi Mshana.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, watuhumiwa hao wakiwa wanatumia gari namba T. 782 BEU aina ya GX 100 T/Cresta na gari lingine lisilokuwa na namba za usajili lenye namba za Chases GX 6011835 aina ya Grand Mark II waliwavamia wafanyabiashara wenye asili ya Kihindi na kuwapora Sh milioni 3.7 na vitu mbalimbali.
“Majambazi hawa waliweka magogo barabarani na kusimamisha gari la Wahindi hao, likiwa linaendeshwa na dereva Ezekia Matatila na kudai gari lao ni bovu kisha kuwapora wahanga fedha hizo pamoja na begi lililokuwa na nguo na vitu mbalimbali, huku wakiwatisha kwa kutumia silaha,” alisema Msangi.
Msangi alisema wakati tukio hilo linafanyika, baadhi ya wananchi walifanikiwa kutoa taarifa polisi ambao walifika kwa haraka na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watano huku mmoja akiwa amekimbia.