MWILI WA SHEIKH WA MKOA WA MARA WAWASILI MJINI MUSOMA




 Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa akiongoza waombolezaji
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kuugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubiri mwili wa shekh Magee wamesema  wamepata pigo kubwa kufuatia msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.

Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa leo kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.
 
Na Augustine Mgendi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo