JAMAA mmoja Ijumaa alikiri hadharani katika mahakama ya Mombasa kwamba yeye ni shoga na anaugua maradhi ya ukimwi.
Amin Mohammed
ambaye anajulikana kwa jina la utani la Amina alisema hayo baada ya
kukanusha shtaka la wizi mbele ya hakimu mwandamizi Samuel Gacheru.
Mtuhumiwa alishtakiwa pamoja na wengine ambao hawakuwa mahakamani na mashtaka mawili ya wizi na kupatikana na mali ya wizi.
Stakabadhi ya
mashtaka inadai kwamba alimnyanganya raia wa Ubelgiji, Bw Jozef
Grzogozz Gradus simu ya thamani ya Sh 84,000 akiwa na wengine ambao
hawakuwa mahakamani.
Kiongozi wa
mashtaka Simon Waithaka aliambia mahakama kwamba Amina alitekeleza kosa
hilo mnamo Januaru 24 katika nyumba ya NSSF iliyoko barabara ya Nkurumah
katikati mwa wa Mombasa.
Bw Waithaka aliambia mahakama kwamba Amina alitumia nguvu dhidi ya Bw Gradus wakati wa kutekeleza kitendo hicho.
Katika shtaka
la pili, Amin alikanusha kupatikana na mali ya wizi ambapo yadaiwa
katika hali ya kutekeleza wizi alijipatia kwa njia ya hila simu aina ya
IPAD.
Stakabadhi ya shtaka lilieleza kwamba amejipatia simu hiyo licha ya kuwa na ufahamu kwamba simu hiyo ilikuwa mali ya wizi.
Malipo
Hata hivyo, mshtakiwa alidaiwa kwamba Bw Gradus alikuwa “mteja wake” na baada ya kushiriki naye ngono, lakini akadinda kumlipa.
“Na mimi
nilikwamilia simu yake baada ya yeye kukata kunilipa. Tulikubaliana
malipo ya Sh 1500,” akaelezea mshtakiwa na kuibua kicheko mahakamani.
Alizidi kudai
kwamba walikuwa na mlalamishi tangu usiku wa kuamkia Ijumaa kabla ya
kukosana baada ya Mbelgiji huyo kudinda kumlipa.
Mshtakiwa
huyo aliambia mahakama kwamba tangu akamatwe hakumeza dawa zake za
kupunguza makali ya maradhi ya HIV/AIDS na kutaka usaidizi wa mahakama
kupata dawa hizo.
Kesi itaendelea kusikilizwa mnamo Februari 6 mwaka huu wa 2014.