Faustine Ruta, Bukoba
Alhamisi
ya leo Daraja la Mto Kanoni linalounganisha Manispaa ya Bukoba na Wilaya
nyingine na pia likitumika kama njia kuu ya kwenda Nchi jirani
limezinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanali mstaafu FABIAN
MASSAWE.
Daraja hili lilikuwa kwenye ukarabati takriabni miezi nane sasa
ambapo watumiaji wa vyombo vya moto walikuwa wakilazimika kupitia kwenye
Barabara ya muda ya Nyakanyasi, Migera au Kashura kuingia katika
Manispaa ya Bukoba.
Limekamilika sasa. Pongezi kwa Tanroads Kagera na karibu Bukoba.
Mkuu
wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE amezindua Daraja la
Kanoni hii leo Asubuhi. Na hapa alikuwa akijiandaa tayari kwa kukata
utepe
Safi....Tayari Uzinduzi
Mkuu wa mkoa wa KAGERA (kulia), Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE amezindua Daraja la Kanoni hii leo Asubuhi.

Viongozi mbalimbali wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika leo asubuhi saa 2:00

Mkuu
wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE (kushoto) akiwa
sambamba na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani leo kwenye
uzinduzi wa Daraja la Mto kanoni
Mkuu
wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe akiteta na Wananchi wa
Bukoba kuhusu Uzinduzi huo akisisitiza swala zima la usafi kwa ujumla.
Mkuu
wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe akiwapungia na
kuwasalimia wananchi wa Bukoba waliohudhulia uzinduzi huo wa daraja la
kanoni hii leo
Mkuu wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE leo kwenye uzinduzi wa Daraja.
Daraja
hili lilikuwa kwenye ukarabati takriabni miezi nane sasa ambapo
watumiaji wa vyombo vya moto walikuwa wakilazimika kupitia kwenye
Barabara ya muda ya Nyakanyasi, Migera au Kashura kuingia katika
Manispaa ya Bukoba.
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani nae alikuwepo kwenye uzinduzi huo
Mkuu
wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe na Viongozi wengine
wakipita juu ya daraja hilo la Kanoni lililozinduliwa hii leo Asubuhi.
Mkuu
wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe (katikati) kulia ni
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani wakipita juu ya Daraja kwa
furaha leo kwenye uzinduzi wa Daraja la Mto kanoni
Pongezi kwa Tanroads Kagera na karibu Bukoba.