![]() | ||
| Mh. Cathy Magige |
Mheshimiwa Cathy, Mbunge wa Viti Maalum
Vijana CCM aliyasema hayo leo kwa simu akiongea na Blogu hii kwamba
ameshitushwa sana na ujumbe wa simu ambao umekuwa ukisambazwa kila kona
ya Tanzania na hata kumfikia Dada yake aliyeko Ohio, ambaye alimtumia
mara moja baada ya kupokea tu ujumbe huo. Pamoja na maelezo mengi sana
yakumtukana Zitto ujumbe huo unasomeka hivi:-
"Hii email itapokewa na zaidi ya watu 50. Nimeifanya makusudi, na kama unabisha haukwenda Dubai na Catherine Magige, niko tayari kuweka scanned copies ticket zenu na video zenu za siri mkiwa huko"
Mheshimiwa Magige, anawaomba wale wanaohusika na kusambaza ujumbe huu mitandaoni na kwenye simu za watu wajitokeze na kutoa ushahidi huo wa Video na copy za Ticket walizosafiria kama ni kweli wanazo ama sivyo waache uzushi huo ambao anasema hauna maana na wala hauna ukweli wowote.

Mheshimiwa
anasisistiza kwamba tatizo lao ni Zitto sasa haelewi ni kwa nini
wanajaribu kuchafua na wengine wasio na makosa kama yeye, anarudia tena
kwa wale wote wanaodai kuwa na huo ushahidi wa yeye kuwa na Zitto,
popote pale watoe ushahidi huo ili ukweli uonekane wazi na wananchi wote
badala ya uzushi usio na maana wenye nia ya kumchafulia jina.