Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akipokea ua kama isharaya
kukaribishwa tena kwenye wizara hiyo, awali dkt. Seif alikuwa Naibu
Waziri kwenye wizara hiyo.
Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii akisalimiana na baadhi ya wakurugenzi wa wizara hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kebwe S. Kebwe akisalimiana na
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando,pembeni ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Charles Pallangyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya
wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, akisalimiana na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Danford Makala.
Dkt.Seif Rashid ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akisaini kitabu kwenye ofisi yake mpya wizarani hapo.
Naibu
Waziri akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi yake mpya mara baada ya
kuripoti rasmi kuanza kutumikia cheo chake kipya kwenye wizara
hiyo.kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Charles Pallangyo.
Baadhi
ya watumishi wa Wizara hiyo wakisubiri kuwapokea Mawaziri wao wapya nje
ya viwanja vya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.( Picha zote na
Catherine Sungura –MOHSW).