skip to main |
skip to sidebar
MAN UNITED YACHEZEA TENA KICHAPO, YAPIGWA 2-1
Fabio Borini akishangilia baada ya kuifungia Sunderland bao la pili kwa njia ya penalti kipindi cha pili dakika ya 64.
Nemanja Vidic wa Manchester United akifunga bao la kusawazisha kwa timu yake na kufanya matokeo kuwa 1-1 katika dakika ya 52.
Sunderland wakishangilia bao lao la kwanza alilojifunga Ryan Giggs dakika ya 45.
Fabio Borini wa Sunderland (kulia) na Patrice Evra wakikwaana wakati wa mechi hiyo.
Timu ya Manchester United imepokea kipigo
kingine cha bao 2-1 kutoka kwa Sunderland katika mechi ya Nusu Fainali
Kombe la Capital One na kuwa mchezo wa tatu kufungwa timu hiyo mfululizo
baada ya awali kufungwa na Tottenham na Swansea katika Ligi Kuu ya
England na Kombe la FA.
Mechi ya marudiano itapigwa Old Trafford Januari
22 mwaka huu.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi