Haya ni maelezo ya shuhuda Mohamde Hamis ambae alikua miongoni mwa abiria ndani ya boti.
1. Boti ilipofika Nungwi sehemu yake ya mbele ilizama na mabegi yake
na iliporudi juu ikazima na kuzunguka palepale, dakika tano baadae
ikawaka ndio tukaondoka watu wengine wakiwa wamebaki kwenye maji
wanaelea.
2. Baada ya boti kuwaka ndio wale watu waliobaki kwenye maji wakatupiwa viokozi vya upepo ndio boti ikaendelea na safari.
3. Hatujui ni watu wangapi waliobaki kwenye maji ila hakuna baharia hata mmoja alieshuka kutoka kwenye boti kwenda kwenye maji.
4. Tulipokaribia bandarini Znz tulitangaziwa kwamba hatutapelekwa
bandarini kushuka mpaka tuvue life jacket tulizozivaa baada ya dhoruba
ili tusionekane nazo manake walitaka habari zisivuje.
5. Wale waliorushwa kwenye maji walichukuliwa na wimbi, watoto na watu wazima nilikua nawaona kabisa wametupwa kwenye maji.
6. Sehemu ya watu walioachwa baharini ni miongoni mwa waliokua
wamelala kwenye sehemu ya boti iliyozama, kina mama na wengine
waliowepesi kutapika ndio ilibidi wakae nje kwenye hii sehemu ili
wapigwe na upepo.
7. Ni ngumu kujua walikua watu wangapi waliokuwemo pale mbele kwenye sehemu iliyozama ila ni zaidi ya 20.
Kwa uthibitisho zaidi unaweza kumsikiliza huyu shuhuda hapa chini..
chanzo:millardayo.com
