Na Ibrahim Yassin,Kyela
KATIKA hari isiyokuwa ya
kawaida kijana Razaro Mwabakiugwe mkazi wa kijiji cha Lupembe kata ya Ikolo wilayani
Kyela mkoani Mbeya anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumfanyia ukatili Lucia
Katule ambaye ni mlemavu kwa kumshambulia kwa makonde na kumsababishia maumivu
makali sehemu ya mwili wake.
Akisimulia mkasa huo mbele ya
waandishi wa habari nyumbani kwake Katuli alisema kuwa tukio hilo lililtokea jana majira ya saa sita
mchana katika kitongoji cha Mikoroshoni kata ya kyela mjini baada ya kijana
huyo kuingia na baiskeli katika varanda ya nyumba wanayoishi na alianzisha fujo
hizo baada ya wapangaji wenzake kumhoji.
Alisema kuwa kijana baada ya
kuhojiwa kuhusu kitendo cha kuigia na baiskeli ndani ya varanda alijibu kwa
kejeli kuwa mbona mlemavu anaingia na baiskeli humu lakini hamumsemi na kuwa
alizidi kuongea kashfa ya kuwa ndiyo maana idi amaini alikuwa anawatupa
baharini watu kama hawa.
Aliongeza kuwa baada ya
kusema hivyo alishuka kwenye baiskei na kuanza kumshambulia kwa ngumi na mateke
hadi kumsababishia maumivu makali ikiwamo kumuumiza mguu wake wa kushoto bila
kujali ulemavu alionao.
Aliendelea kusema kuwa baada
ya hapo wasamalia wema walimuokoa na kumkibiza katika kituo cha polisi wilaya
ambao walimpatia RB Iliyomuwezesha kwenda kupata matibabu katika hospitali ya
wilaya ya Kyela ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Mwenyekiti
wa kitongoji cha
Mikoroshoni Kalison Bongo alisema alikiri kuwepo na tukio hilo
na kudai kuwa alifuatwa na wasamalia wema ofisini kwake na kujurishwa
tukio hilo ambapo alifika eneo la tukio kwe lengo la kupata
ufumbuzi juu ya tukio hilo.
Alisema alipofika katika
nyumba hiyo hakumkuta mtu na ndipo wapangaji wengine walimueleza kuwa mama
aliyeshambuliwa alikimbizwa hospitalini na kijana aliyeshambulia amekimbilia
kusiko julikana mara baada ya kufanya kosa hilo na kuwa alitoa maagizo kuwa iwapo
atakuja afike katika ofisi yake. ndani ya siku tatu.
Aliongeza kuwa iwapo hatafika
katika ofisi yake ndani ya siku tatu ataungana na jeshi la polisi kwa ajili ya
kumsaka popote alipo ili afikishwe katika mikono ya sheria ili aweze
kuadabishwa kwa mujibu wa sheria na itakuwa ni fundisho kwa vijana wengine
wenyetabia kama hiyo.
