MAJANGA:. MAMA ATELEKEZA WATOTO JIJINI DAR, AENDA KUOMBA

Watoto walioachwa na mama yao wakiwa wamelaa eneo la makutano ya barabara ya Zaramo na Jamhuri jijini Dar.
KATIKA hali ya kusikitisha kamera yetu mchana huu imenasa picha za watoto waliosemekana kuwa mama yao aliwaacha na kwenda kuombaomba katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Watoto hao walioonekana kuwa na njaa kali walikutwa katika eneo la makutano ya barabara ya Zaramo na Jamhuri jijini Dar.
Mpaka mwanahabari wetu anaondoka eneo la tukio mama huyo alikuwa bado hajarudi na haikujulikana atarudi saa ngapi.
(PICHA / HABARI: HARUNI SANCHAWA / GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo