Stori: Chande Abdallah na Denis Mtima, Mwanza.
UONEVU! Bibi kizee, Mwamini Abdallah anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100 (alikuwepo wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia ya 1914), anadai kunyang’anywa shamba na ndugu zake kisha kutelekezwa na kumsababishia kuishi kwa tabu.
UONEVU! Bibi kizee, Mwamini Abdallah anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100 (alikuwepo wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia ya 1914), anadai kunyang’anywa shamba na ndugu zake kisha kutelekezwa na kumsababishia kuishi kwa tabu.
Akizungumza na waandishi wetu, bibi huyo anayeishi katika Kijiji cha
Ngeleka-Usagara mkoani hapa alidai kwamba aliingia kwenye mgogoro wa
mirathi na ndugu zake aliochangia nao baba mara baada ya mzazi wake
huyo kufariki dunia.
Bibi huyo alisema kuwa mgogoro huo ulisababisha kufunguliwa kwa kesi
Mahakama ya Mwanzo ya Misungwi na hukumu kuwapa haki ndugu zake hao na
yeye kuambulia ardhi kidogo.
Hata hivyo, aliiuza ardhi hiyo kidogo aliyopewa baada ya kukosa huduma za msingi mara alipotengwa na ndugu zake.
Waandishi wetu wamejionea hali ya bibi huyo ambaye analala chini
akitandika na kujifunika magunia huku paa la ‘kibanda’ anachoishi
likivuja.
Kikongwe huyo anapata msaada kidogo kutoka kwa jirani yake Halima Said anayemchotea maji na kumpatia akiba kidogo ya chakula.
Alisema kuwa hata kibanda hicho cha matope anachoishi kwa sasa
alijengewa na mama mmoja aliyekuwa nesi maeneo hayo lakini kwa sasa
kipo hatarini kubomolewa kutokana na kujengwa kwenye hifadhi ya barabara
inayotengenezwa kutoka Usagara kwenda Kisesa.
“Nalelomba bhamunhu mnahmbilije naphandike hakulalaa niishiliwa,”
alisema bibi huyo kwa Lugha ya Kisukuma akimaanisha ‘naombeni mnisaidie sehemu ya kulala na chakula.’
Kufuatia ugumu wa maisha ya bibi huyo, mjukuu wake, Mariam John (15)
ndiye anayemsaidia kwa kufanya kazi za ndani Mwanza mjini kwa ujira wa
Sh. 20,000/= kwa mwezi, fedha ambazo pia hazikidhi mahitaji yao binafsi.
Kwa yeyote atakayeguswa na mateso anayopata bibi huyu na anataka
kutoa msaada wake, awasiliane na mwanaharakati wa kutetea haki za
binadamu wa asasi ya FARIJIKA kwa namba 0787 040 261 au 075 604 026.
CHANZO: GPL