KIJIJI CHA TANDALA WILAYANI MAKETE MBIONI KUJENGA OFISI YA KIJIJI

Kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe kinatarajia kuanza ujenzi wa ofisi ya Mtendaji wa kijiji kutokana na ukosefu wa jengo la ofisi ya kijiji kwa muda wa miaka mingi ambapo hivi sasa linatumika jengo la posta Tandala kama ofisi ya kijiji.

Ujenzi huo unaanza mapema mwaka huu eneo la mtaa wa Singida  ambapo mpaka kufikia sasa uwanja umepatikana tayari  kwa ujenzi kuanza.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Afisa mtendaji wa kijiji hicho ambaye pia ni kaimu Afisa mtendaji kata ya Tandala Bw.Ambele Sanga (pichani) amesema kuwa ofisi hiyo itaanza kujengwa mapema mwaka huu

Amesema kuwa kila kitongoji kinatakiwa kuchangia nguvu kazi ikiwemo kufyatua tofali 1500 ili ziweze kutumika katika ujenzi huo na kusema kuwa kijiji hicho kinavitongoji 6

Pia amevipongeza vitongoji ambavyo tayari vimekwisha kuaandaa tayari tofali ikiwemo kitongoji cha Utsewa na Lwangilo 

Katika hatua nyingine Bw.Sanga amesema kuwa wanampango wa kujenga Intenki katika mradi wa maji Utsewa pamoja na kuboresha miundombinu ya kitongoji cha Utsewa na kilovoko ikiwa ni pamoja na kutoa miti ya kigeni na kupanda miti ya asili katika vyanzo vya maji

Na Henrick Idawa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo