Mchezaji wa Juan Mata amewasili jijini Manchester katika dimba la
Carrington tayari kufanyiwa vipimo na timu yake mpya ya Manchester
United.
Mata amejiunga na United baada ya timu hiyo kuvunja rekodi ya ada ya
usajili kwa kukubali kulipa kiasi cha paundi millioni 37 ili kupata
saini ya mchezaji huyo wa kihispania. Aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi
wa Manchester United kwa kutumia helkopta aliyokodishiwa kutoka jijini
London.
Wachezaji wa United Rio Ferdinand na Robin Van Persie walitumia
akaunti zao za Twitter kumkaribisha kiungo huyo ambaye anategemewa
kusaini mkataba wa miaka mitano huku akilipwa kiasi cha paundi 150,000
kwa wiki.