BAADA YA KUTIMULIWA. MWIGAMBA AAPA KUILIPUA CHADEMA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, ameapa kuwashangaza viongozi wa chama chake na kwamba amejipanga kufanya kitu kikubwa katika siku chache zijazo.

Mwigamba ambaye hivi karibuni alifukuzwa uanachama pamoja na aliyekuwa mshauri wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk. Kitila Mkumbo kwa tuhuma za usaliti, alisema anashangazwa na uongozi wa chama hicho kutokuwa na onyo kwa wanachama wake na badala yake wamekuwa ni watu wa kufukuza fukuza tu.

Mwigamba alisema anajiamini na anaamini kuwa waraka waliouandaa na haukuwa na nia ya kukibomoa chama. Aidha, alibainisha kuwa alishajua kwamba atafukuzwa ndani ya CHADEMA na kwamba alishajipanga kwa ajili ya kufanya maajabu yatakayowashangaza wengi ndani ya CHADEMA.

“Nitawa-surprise CHADEMA soon …. nimejipanga, mimi wasinifananishe na wale ambao walifukuzwa kabla yangu.

Mimi si mjinga, sasa nitafanya maajabu. Kama niliweza kuandaa mkakati huo wa mabadiliko ambao uliwashtua viongozi wa CHADEMA na hata kuitikisa nchi, ni wazi nina akili za kutosha na kwamba ninachosubiri ni muda tu,” alisema Mwigamba kwa kujiamini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo