WATOTO YATIMA KITUO CHA MOYO KWA MOYO IRINGA KUFANYIWA HARAMBEE

 
Mratibu wa Harambee Meneja wa miradi wa kituo cha Moyo kwa Moyo, Renatus Mpiluka akizungumza kuhusu harambee katika ofisi za kituo hicho mjini Iringa.
Consolata Sanga meneja wa fedha wa CPEC kushoto , Renatus Mpiluka meneja mradi na Destory Wikedzi  Mkurugenzi wa CPEC wakiwa katika picha ya pamoja katika ofisi hizo (Picha zote na Denis Mlowe)
=========  ==========   ==========
WATOTO YATIMA KITUO CHA MOYO KWA MOYO KUFANYIWA HARAMBEE

Na Denis Mlowe,Iringa

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Creating Partnerships to Empower Communities (CPEC) la Iringa kwa kushirikiana na kituo cha radio cha Nuru Fm wameandaa harambee ya kukichangia kituo cha watoto yatima cha Moyo kwa Moyo kilichoko Matanana wilayani Mufindi.

Akizungumza na Tanzania Daima mratibu wa Harambee hiyo na Meneja wa Miradi wa kituo hicho Renatus Mpiluka alisema lengo la harambee hiyo ni kutunisha mfuko wa kituo hicho ili kuboresha huduma kwa yatima wapatao 300 wanaohudumiwa na kituo hicho.

Mpiluka alisema wameamua kufanya harambee hiyo kwa kuwa waliokuwa wafadhili wa kituo hicho kutoka Sweden wamepunguza misaada zaidi ya asilimia 70 kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani.

Alisema watoto yatima wanamahitaji makubwa ya ada za shule kwa wanafunzi wanaenda shule za sekondari, mavazi, chakula hivyo inawawia vigumu kituo kumudu gharama za uendeshaji wa kituo hicho.

“Kituo kinakumbana na changamoto nyingi sana tangu wafadhili kupunguza msaada hivyo tumeamua kufanya harambee ili tuweze kujiendesha na kuwasaidia watoto hao yatima ambao kwa kweli ni wengi na ni jukumu letu kuweza kuwasaidia kwa hali na mali katika kufanikisha ndoto zao za miasha” alisema Mpiluka

Mpiluka alisema changamoto hizo za mahitaji makubwa ya watoto yatima zimepelekea kituo cha Moyo kwa Moyo  kushirikisha wadau mbalimbali katika kuchangia na kujitolea misaada mbalimbali kwa kituo hicho.

Alisema kituo kimefanikiwa kuwapatia mafunzo ya ufundi watoto yatima na kuwawezesha kusoma masomo ya komputa na hivyo wafikishapo miaka 18 waweze kujitegemea na kuwapatia huduma ya chakula watoto walioko katika shule za msingi za Mufindi.

Katika harambee hiyo itakayofanyika siku ya Krismasi,Mgeni rasmi anatarajia kuwa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga na kusindikizwa na bendi ya Whispers  ya jijini Dar es salaam.

Kwa yoyote anayetaka kuchangia katika harambee hiyo anaombwa atume kwa tigo pesa 0655161678 na M-pesa 0756 56 56 03 au kwa kiingilio cha shilingi 20,000 kwa VIP na wakubwa 5000, watoto 2000. Kumbuka Kutoa ni moyo usambe si utajiri


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo