UCHAFU NDIYO SABABU YA KIVUKO CHA MV MAGOGONI KUZIMA KATIKATI YA SAFARI

Uchafu unaotupwa baharini hasa wa mifuko ya plastiki ndiyo uliosababisha kuzima ghafla kwa injini ya Kivuko cha Mv Magogoni katikati ya wiki hii.
 
Akizungumza jana kuhusu hali hiyo, Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray alisema kuwa mafundi baada ya kuchunguza injini nne za kivuko hicho, walibaini kwamba zimejaa taka. 
 
“Propela zilivuta maji yenye uchafu mbalimbali na hivyo injini zikashindwa kufanya kazi vizuri. 
 
Mafundi walitoa uchafu wakaifanyia marekebisho na kuijaribu kwa dakika kama 20,” alisema Mziray.
 
Alisema kuzima ghafla kwa injini kulizua hofu kubwa kwa abiria, ingawa hawakuwa katika hali ya hatari kwa sababu meli ikizima katikati ya maji haizami.
 
“Tumebaini kuna haja ya kutoa elimu ya usafiri wa majini kwani hofu ya abiria ingeweza kusababisha maafa makubwa.CHANZO MWANAINCHI


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo