MAJONZI MAKUBWA:RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

Habari za uhakika kutoka nchini Afrika kusini zinasema kwamba, Rais wa zamani wa Afrika Kusini ameaga dunia . 

Mandela ameaga Dunia akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa jela kwa miaka 27

Mandela alikua anpokea matibabu ya homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu. Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Rais wa taifa hilo, Jacob Zuma , alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.

Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kua mwanawe wa kume alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.


Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.


Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.


Hakuonekana sana hadharani tangi alipostaafu mwaka 2004.


BBC


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo