MTOTO WA SIKU 7 AOKOTWA AKIWA HAI RUVUMA



MTOTO wa siku saba ambaye ameokotwa maeneo ya Mateka akiwa ametupwa jalalani anahitaji msaada wako.
Aidha amesema anayetaka kusaidia anaweza kupiga simu 0755061588 kwa maelekezo zaidi.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Benedict Ngaiza ambaye hospitali yake kwa sasa ndiyo inamtunza mtoto huyo amewataka wanawake kujiepusha na vitendo vya ukatili hasa kwa watoto kwa kujiunga na uzazi wa Mpango.

Akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Peter Kiula,amesema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vina zidi kukithiri na anaamini inatokana na wanawake kubeba Mimba bila Maandalizi.

Naye muuguzi  Anna Chaula katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma amewaomba wana wake kushirikiana na Vyombo vya Dola kumbaini mama aliyemtupa Mtoto kwa kuwa wanao fanya vitendo hivyo ni wale tunao ishi nao.

Naye Makamu mwenyekiti wa Mtandao wa Police wana wake, mkoani Ruvuma Fadhila Chacha amesema Mtandao wa Police wanawake unaendelea kupambana na vitendo vya ukatili,Ndiyo Maana kila wakati huokoa uhai wa watoto.

Mkoa wa Ruvuma wakati ukiwa katika kilele cha siku 16 za kulaani vitendo vya ukatili dhidi ya mama na Mtoto tayari watoto watatu wameokotwa jalalani na mmoja kuliwa na mbwa eneo la mfaranyaki baada ya kutupwa .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo